Tarehe 8 mwezi wa 10 mombasa itapata msisimko wa burudani (mombasa festival)burudani hioo itakua na wasanii wawili wa kimataifa pia ni marafiki wakubwa sana wasanii hao ni Chris brow kutoka marekani na wizkid kutoka Nigeria hivyo mombasa wajiandaee
Jumanne, 27 Septemba 2016
Mafufuli alipongeza kanisa la anglicana
Raisi john pombe magufuli amelipongeza kanisa la anglicana kutokana na kuvutiwa na jinsi wanavyo endesha ibada .Magufuli alifika hapo kanisani jumapili ili kwa kushtukiza na kusali nao misa ya kwanza na pia alitoa zawadi ya milioni moja kwa wana kwaya
Alikiba apasua anga
Msanii alikiba amezidi kupasua anga kimataifa baada ya kutajwa kwenye kuwania tuzo za Mtv ema akishindana na black coffie wizkid olamide na casper nyovest .kiba kapata nafasi hio ambapo kamzidi mpinzani wake diamond platnumz toka arudi kimuziki inaonyesha kiba anataka heshima yake ya ufalme wa bongo flavour tena hivyo tumpigie kura ili alete tuzo nyumbani Tanzania
http://base.mtvema.com/vote#cat=best-african
Jumatatu, 26 Septemba 2016
Tekno waleta phantom 6
Campuni ya simu za mkononi Tekno wamezindua simu mpya aina ya phantom 6 simu hizo zilizinduliwa juzi usiku huku uzinduzi huo ulihudhuriwa na msanii kutoka Tanzania Alikiba pamoja na mtangazaji maarufu millad ayo ambao walialikwa kwenye uzinduzi huo.
Jokate azidi kujiwekeza
Mwanamitindo marufu jokate mwigelo kutoka Tanzania amezidi kuongeza brand yake kwa kutafuta wasusi wa mitaani na kuchagua wachache ambao ataweza kufanya nao kazi hioo ni kwa dar nzima pia dada huya alijiwekeza kwenye mambo ya ndara (snikers) .
Alikiba atoa ofa dance mia mia
Msanii alikiba atoa ofa ya kuchukua madancers walioshiriki kwenye dance mia ili aweze kufanya nao kazi kwenye shoo zake hivyo amesema atachukua baadhi ya madancer hao pia alikiba kama tunavyojua kuwa atatumbuiza kwenye jukwaa la mtv huko south Africa
Jumatatu, 19 Septemba 2016
Watanzania wapata ajali zambia
Ajali.imetokea zambia ambako basi la power tools limepata ajali inakadiriwa kuwa abiria 62wamefariki basi hilo lililokua linatoka nakonde kwenda kitiwe ni watanzania wengi wamefariki
Kwa habari zaidi endelea kuwa karibu na blog yetu pendwa
Jumapili, 18 Septemba 2016
Diamond ,Rayvanny wamlipa Alikiba na baraka
Msanii Diamond platnumz ameachia nyimbo yake aliyomshirikisha Raymond ambae ni msanii wake hii imeonekana kama ni kumlipa alikiba aliye imba na baraka the prince
Jumamosi, 17 Septemba 2016
Arsenal,Manchester city,Lecister city hatari tupu
Team ya Arsenal jana iliendeleza ushindi baada ya kuifunga hull city goli 4-1 huku man city ikishinda 4-0 lecister ikashinda goli 3-0
Diamond ,Alikiba kumbe walishawahi kukutana studio
Wasanii mahasimu Diamond platnumz na mpinzani.wake Alikiba (king kiba) inasemekana wapiwahi kukutana studio mwaka jana na aliyewakutanisha ni msanii neyo abaye alitaka wafanye kolabo ya watu watatu ila alikiba hakupendezwa na hilo hivyo neyo aliamua kufanya na diamond tu kisha akakataa kufanya na alikiba ila kwa mujibu inasemekana kuwa msanii huyo alikuwa hajui bifu la wawili hao ila baadae alimtafuta alikiba huko Uganda na kumuomba samahani kwa yaliotokea na kuamua kufanya nyimbo.na Alikiba.
Jokate asaidia wathirika wa janga la tetemeko kagera
Mwanadada mwanamitindo marufu nchini Tanzania dada jokate mwigelo (jojo) amewasaidia wathirika wa tetemeko la ardhi huko kagera jana baada ya kwatembelea kutokana na kuguswa na maafa hayo
Yanga kiboko simba jeuri
Yanga jana iliendeleza ubabe wake baada ya kuifunga mwadui fc goli 2-0 mwadui inayongozwa na kocha mwenye majigambo jamuhuri kiwelo yanga ikiwa na kocha plujim magoli ya yanga yalifungwa na Tambwe ambae ameanza kukipigania kiatu chake cha dhahabu na lapili lilifungwa na donald ngoma huku yanga ikibaki kuwa timu pekee ambayo haijaruhusu goli .Nao mahasimu wao simba sc jana walionyesha kuzidi kulipania taji la ligi la msimu huu baada ya jana kuifunga Azam fc goli 1-0 goli lililofungwa na winga shiza kichuya aliyesajiliwa kutoka mtibwa simba kwa sasa ipo kileleni kwa point 13 ikifuatiwa na yanga yenye point 10 huku ikiwa na kiporo kimoja
Fiesta yazidi kupamba moto mikoani
Tamasha kubwa la muziki linalofanyika nchini limezidi kupamba moto mikoa mbali mbali na leo lipo morogoro
Alhamisi, 15 Septemba 2016
Serengeti boys dimbani
Timu ya vijana ya Tanzania Serengeti boys itashuka dimbani tarehe 18 kwenye uwanja wa taifa ikiwa inacheza ba vijana wenzao kutoka congo kwenye hatua ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya africa ya vijana hivyo tuwape support vijana wetu
Jumanne, 13 Septemba 2016
Bungeni
Kikao cha 6 mkutano wa 4 bunge la 11 limeanza bungeni mjini dodoma huku kikao hicho kikiongozwa na Mh.Musa Hassan zungu
Vijana 33 wakamatwa
Vijana 33 wamekamatwa kwa makosa ya kuwalaghai waschana huko beach na wengine wakifanya nao mapenz hivyo jeshi la police limeonya vitendo hivyo ili kutodhalulisha wasichana
Waziri mkuu azidi kwajali wahanga kagera
Waziri mkuu majaliwa amezidi kutafuta msaada wa kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi huko kagera kwa kukusanya bilioni 1.3 ili kusaidia wahanga hao kwa habari zaidi endelea kufuatilia ukurasa wetu huu
UEFA moto umewaka
Jana kulikua na mechi kali za UEFA champion ligue ambazo team zilizocheza zilititimuana kivumbi ili kuongoza ligue team ya Barcelona ilifumua celtic bao 7-0 huku mesii akiandika historia ya kuwa na hatrick sita kwenye uefa na kumpiku mpinzani wake Ronaldo pia Arsenal iliponea baada ya kuchomoa goli dakika ya 77kupitia kwa fundi wao sanchez na mchezo ulisha kwa suluhu ya 1-1 matokeo mengine 👇👇👇
Mugabe Ajengewa sanamu
Raisi wa nchi ya zimbabwe robert mugabe amejengewa sanamu mbili huko nchini kwake na sanamu hizo zimezinduliwa leo
Swali je kwa sasa tanzania ungependa nani afanyiwe hivyo jibu hapo chini
Alikiba azidi kutanua mombasa na Mr Gavana
Msanii alikiba amezidi kuthibitisha kuwa yeye ni kipenzi cha watu baada ya kuendelea kubaki mombasa ambako alikua amekwend kufanya shoo .Alikiba baada ya kufunika kwenye shoo pia amepata bahati ya kulala ikulu kwa gavana joho wa mombasa huku akila idi huko huko na kusherekea mambo mengine picha zilimuonyesha kiba akila bata na mheshimiwa joho baharini
Baraka achia nyimbo na alikiba
Jumatatu, 12 Septemba 2016
Ali kumaliza mwaka na nyimbo Tano.
Msanii Alikiba amesema kuwa atatoa nyimbo ndani ya hii miezi mitatu iliyobaki kama tunavyojua kuwa Alikiba nyimbo zake hudumu kwa muda mrefu na swali ni je hizo nyimbo ni kali zaidi ya Aje nyimbo hizo zitakua ni colaboration na zingine za kushirikishwa na zingine zake mwenyewe pia nyimbo zinazo hisiwa kati ya hizo tano ni Nisamehe ya baraka the prince ft Alikiba pia Aje remix ft mi mbaga na nyingine akiwa na dimpoz ila jina bado hatuna uhakika kwa sababu.alisema ni hashtag na siku hizi tunaona anatumia Kajiandae hizo mbili nyingine hazijafahamika ila hatujui kama Avelina ipo kumo pia kaa karibu nasi ili uzidi kupata hizi story
Baraka the prince ft alikiba nisamehe kesho inatoka
Jumapili, 11 Septemba 2016
Alikiba Ataperfome kwenye tuzo za MTVmama 2016
Msanii Alikiba (king kiba)ametajwa leo kuwa ataperfome live kwenye tuzo za MTV Africa awards ambazo zitafanyika October 22 huko nchini south Africa .Alikiba kapata nafasi hio baada ya kuwapiku wapinzani wake watatu Diamond platnumz ,sauti soul na eddy kenzo .Alikiba alipata kura Asilimia 45 akifuatiwa na Diamond asilimia 42
Ila tuseme hongera kwa Alikiba
Mziki wa Tanzania unazidi kufika mbali
Magufuli agahiri kutoka nchini
Raisi wa Tanzania john pombe magufuli ameghairi kuenda nchini zambia kwenye kuhudhuria kuapishwa kwa raisi mpya nchini humu kwa mujibu wa vyombo vyetu vya habari vinasema magufuli ameghairi kwa sababu ya kutaka kushuhulukia maafa ya tetemeko la ardhi huko kanda ya ziwa na kuaababisha vifo vya watu 16 hivyo kwenye sherehe hizo atakwenda mheshimiwa mama samia suluhu .
Wahindi wafanya sherehe wafunga barabara ya posta kwa mda
Wahindi wanaoishi Dar es salaam leo walikua wakisherekea sherehe za holy yani (kupakana unga unga)hivyo walikua wakitembea kutokeaa muhimbili mpaka barabara ya posta nk wahindi hao walikua na mdoli aliyesadikika ni mungu wao .
Baraka the prince anakuja na nisamehe
Msanii anaekuja kwa kasi kuiteka Africa baraka the prince aliye chini ya lebel ya Rockstar 4000 ameahidi kutoa nyimbo yake ya nisamehe aliyomshirikisa msanii mkongwe wa bongo fleva Alikiba (king kiba) ambae wapo nae lebel moja .Baraka amesema nyimbo hio itatoka tarehe
13.9.2016 itakua ni video yake ya kwanza kufanya south Africa so tunaisubiri kwa hamu
Diamond & Kiba waiteka kenya
Wasanii wawili kutoka Tanzania Diamond na alikiba jana usiku waliteka kenye mjini mombasa uwanja wa mama ninga ambapo kulikua na mkutano wa chama cha ODM Gavana wa jiji la mombasa aliwalika wasanii hao kupiga show hapo baada ya kumaliza mkutano wa chama .Diamond ndiye aliyekua wakwanza kuanza kuzikonga nyoyo za wakenya kisha alikiba akafunga kazi akiwa na mdogo wake Abdukiba
Jumamosi, 10 Septemba 2016
Yanga yaendeleza ubabe
Team ya yanga imendeleza ubabe wa kutokufungw ligi toka imeanza msimu huu.yanga imeshinda mechi mbili na kudroo moja hivyo kuifanya yanga kufikisha point 7ikiwa bado inakiporo kimoja leo yanga imeifunga majimaji goli 3-0 magoli yalifungwa na deus kaseke na mshambuliaji Amis Tambwe akifunga mawili huku maji maji hawakuambulia kitu . Msimamo wa ligi 👇👇👇
Arsenal kidedea
Team ya soka ya arsenal kutoka jijini london leo imeweza kushinda kwa bao la jioni baada ya kupata penalt iliofungwa na sant carzola badaa ya mchezo kwenda sare kipindi cha kwanza southamton waliongoza kwa kupata bao la kujifunga kwa cech kutokana na faulo iliyopigwa na Tadic hata hivyo Arsenal hawakukata tamaa wakaendelea kujipanga wakasawazisha goli kupitia captain wao koshenly kwa bao la tiktak kisha kufunga hilo la penalt na kufanya matokeo kuwa 2-1 arsenal imepanda mpaka nafasi ya Tano
Tusubiri matokeo ya michezo ya kesho matokeo mengine ni 👇👇👇
Bunley 1-1 hull city
Bornemouth 1-0 west brom
West ham 2-4 watford
Middelsbrough 1-2 crystal palace
Stoke city 0-4 Totenham hotspurs
Tetemeko la ardhi kagera
Mkoa wa kagera umekumbwa na mafaa ya tetemekola ardhi lililodumu kwa dakika moja na kufanya nyumba kubomoka pia watu kufukiwa na vifusi na wengine kugongwa na magari wakati wakikimbia tetemeko hilo nyumba nyingi zilizo bomoka ni zile zilizojengwa milimani hivyo mpaka sasa watu wanazidi kufikishwa hospitalini mkoani humo
Kwa tarifa zaidi endelea kufatilia blog yetu
Manchester city kileleni
Team ya Manchester city imendelea kubaki kileleni baada ya kifunga team ya Manchester united huu ni mchezo wa kwanza morinho anapoteza akiwa kocha wa man united. Goli la kwanza lilifungwa na mchezaji kelvin de bruyne dakika ya 16 ya mchezo na kuifanya man city kuongoza kwa goli moja kisha dakika ya 36 kelechi iheanacho alipa man city goli la pili baada ya kumalizia mpira uliogonga mwamba uliopigwa na de bruyne kisha man u ikajipatia goli lake la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wake ibrahimovic dakika ya arobaini na kufanya mchezo huoo kuisha kwa goli 2-1
Edited by moraki
Diamond platnumz &alikiba stage moja
Wasanii diamond platnumz na Alikiba watapanda kupiga show mombasa kenya kwenye show ya chama cha ODM (odinga ) kikitimiza miaka kumi ila kwa tarifa zilizo fika ni kua wasanii hao walikataa kulala hoteli walizo pangiwa hivyo hatujui je watakubali kupanda stage moja mana kila moja hakujua kuwa wamepangwa shoo moja
Kwa tarifa zingine endelea kufatilia blog yetu hii ya morakimo.blogspot.com
Hudson kamoga kuteuliwa mkurugenzi
Mtangazaji wa chanel ya clouds tv bwana hudson kamoga ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri
Ya wilaya ya mbulu hivyo ni hatua kubwa sana na ndiye mtangazaji pekee aliye pigiwa simu wakati akiwa kwenye kipindi cha clouds 360 na magufuli
ALL THE BEST BROTHER
Edited by moraki
Shilole na nuh mziwanda fiesta imoo
Hii ni baada ya kukutana kwenye fiesta msanii shishi baby shilole na aliye kua mwandani wake nuh mziwanda wakati wakiwa kwenye gari shilole alikua akimuliza nuh kuwa je anamuogopa nuh akajibu hapana hivyo wasanii hao walikumbatiana na kupigana mabusu kuonyesha hakuna ugomvi
Msanii wa bongo movies azidi kuteka tz
Msanii wema sepetu wa bongo movie azidi kuiteka Tanzania kupitia kujikita kwenye uandaji wa show za kisingeli,baikoko nk hivyo inaonekana inamuingizia sana wema kipato baada ya kumaliza dar sasa ameipeleka show hioo Tanga !!!
Edited by moraki